Pages

Subscribe:

Wednesday, June 29, 2016

JENNIFER HUDSON ASAIN RECORD DEAL NA EPIC RECORDS

Baada ya kufanya perfomance maalum ya kumuenzi  Prince ,mkongwe wa muziki wa soul, perfomance aliyofanya wakati wa utoaji wa tuzo za BET zilizofanyika jumapili ya June 26-2016, staa wa miondoko ya Pop na R&B Jeninifer Hudson amesaini record deal na Epic Records, miongoni mwa...
label kubwa za muziki duniani ambapo mwanamuziki huyo atajumuika na mastaa wengine ndani ya label akiwemo Mariah Carey,Jennifer Lopez na mabinti wa kundi la Fifth Harmony.
epic on hudson 002
Wakurugenzi wa label hiyo wakiongozwa na L.A Reid na Clive Davis watahusika katika maandalizi ya ya album mpya ya mrembo huyo ambae mbali na muziki pia ameshiriki kwenye filamu kadhaa ikiwemo tamthilia maarufu ya ‘EMPIRE’.
hudson post on epic records 007
“Jennifer Hudson is the defining voice of this generation,” ….. “Her award-winning presence on records, in film, and on stage establishes her as one of the premiere artists to emerge in this century”……”I’m enjoying collaborating with my friend and mentor Clive Davis on Jennifer’s first Epic album and excited for her fans to hear what we’re up to…all will be revealed soon!”.Alisema Mkurugenzi mkuu wa Epic Records,L.A. Reid.
 
Mpaka sasa Jennifer Hudson ana album tatu,ikiwemo ‘Self-titled’ iliyotoka mwaka 2008,’effort I Remember Me’ iliyotoka mwaka 2011 chini ya music label ya Arista na ‘JHUD’ iliyotoka mwaka 2014.

Hata hivyo haijafahamika tarehe rasmi ya kutoka kwa album yake mpya chini ya Epic Records.

0 comments:

Post a Comment