Pages

Subscribe:

Friday, March 24, 2017

SHERIA: HIZI NDIYO HAKI ZA MPANGAJI NA MPANGISHAJI NCHINI TANZANIA


Image result for LAW  Mkataba wowote ili utambulike kisheri ni vema zaidi ukapitia kwa wakili anaye tambulika kisheria ili kuupa mkataba wenu nguvu maana yake at list uwe umegongwa muhuri unao tambulika kisheria na mihuri inapatikana kwa wanasheria wanao tambulika kisheria. 

Yoyote aliye ktk mkataba huo anaweza kuuvunja either kwa njia zifuatazo;notice,surrender,disclaimer,frustration,merger e.t.c. Pia njia zote hizo lazima ziangaliwe kwa makini ili...
kuendana na yale yaliyoandikwa kwenye mkataba km.kuheshim clauses mf.pesa ikilipwa hairudishwi hivo loss lies where it falls  

Haki za mwenye nyumba:
Kulipwa kodi yake kutokana na mkataba unavyosema baina yenu, kuingia na kukagua nyumba kwa ruhsa ya mpangaji.


Wajibu wa mwenye nyumba: Ni kuhakikisha nyumba anayopangisha ni nyumba ambayo inafaa kukalika, mfano ina choo iko katika hali nzuri sio imebomoka kiasi haifai kukaliwa na binadamu, wajibu wa kufanya matengenezo makubwa katika nyumba kama ktk mkataba hamkukubaliana kuwa itakuwa matengenezo ya mpangaji, wajibu wa kulipia kodi za serikali za nyumba hiyo kama haiko katika makubaliano na mpangaji.


 Biashara utakayofanya iwe ambayo mmekubaliana na mwenye nyumba wakati unapanga ukibadilisha kama hatoridhika nayo ana haki ya kusitisha mkataba wako mf. Umepanga ili uendesha duka la vifaa vya shule, mara umebadilisha unaweka baa ya kunywa pombe za kienyeji na unasababisha wapangaji wengine wenye biashara zao kutoridhika na biashara hiyo mpya.
Haki za mpangaji:

Kuishi katika nyumba aliyopanga bila kubugudhiwa na mwenye nyumba,

Wajibu wa mpangaji:
Kulipa kodi kama walivyokubaliana na mwenye nyumba, kuishi katika nyumba anayokaa bila kuichafua kiasi cha kufanya hiyo nyumba isikalike na mtu mwingine, kutopangisha mpangaji mwingine bila makubaliano maalum na mwenye nyumba akiondoka, kulipia matumizi mbali mbali ya umeme na maji, simu kama vitu hivyo vipo na havikuainishwa kwenye mkataba kuwa viko katika kodi, wajibu wa kutobadilisha sura ya jengo alilopanga bila idhini ya mwenye nyumba na akiondoka hatakiwi kubomoa kiasi cha kuharibu jengo aliloliacha, wajibu wa kuhakikisha unachokifanya hakiwaudhi wapangaji wengine, wajibu wa kulipia kodi za serikali za biashara unayoifanyia hapo mahali.

Serikali inaruhusu nyumba yeyote bora iwe na huduma muhimu za binadamu kama maji, choo, na mazingira masafi ya kufanyia biashara. Lakini pia eneo hilo liwe limeruhusiwa kwa biashara hiyo unayoifanya. Mf. huwezi kuweka baa eneo la shule ni makosa. Au ukaweka kituo cha kuuzia mafuta wakati watu wanaishi kwenye nyumba hiyo hiyo au kiwanda ukajenga sehemu ambayo imetengwa kwa ajili ya mambo mengine.

Malipo ni makubaliano ya mwenye nyumba na mpangaji. Lakini vigezo vifuatavyo ndio vya kuzingatia. Jinsi ya kulipa kodi - kwa siku, wiki, mwezi au mwaka n.k., au malipo kwa ukubwa wa eneo, mita za mraba, kwa chumba nk.


Awali  ya yote  ni  vema  kufahamu  kuwa  suala  la upangaji na upangishaji  linaongozwa  na sheria  ya  ardhi.  Hii  ni  kwasababu  upangaji  unahusu  nyumba  na  wakati  mwingine  ardhi  isiyo  na  nyumba.  Kwahiyo  niseme tu  kuwa yeyote  anayetaka  kujua  haki  za  kupanga na  kupangisha  basi  na  asome  sheria  ya  ardhi .

1.UKIPOKEA  HELA  YA  MTU  ULIYEMSAIDIA  MAKAZI  ANAGEUKA  KUWA  MPANGAJI  WAKO.

Unapomweka  mtu  katika  ardhi  yako  kwasababu  yoyote  ile  iwe  anakulindia  eneo  lako  au  ndugu  tu  umeamua  kumsaidia    ni  vema  kujiepusha  na  kupokea  hela  yake  yoyote  ikiwa  hutaki   awe  na  hadhi  ya  upangaji.  Unapopokea  hela  za  mtu  kama  huyo   basi  mtu  huyo  kisheria   sio  kwamba  umemsaidia  makazi   tena  isipokuwa  anageuka  na  kuwa   mpangaji  wako  na  hivyo  anastahili  haki  zote  za   kiupangaji.   Ili  mtu  asiwe  mpangaji  katika  ardhi  yako  basi  usipokee chochote  kutoka  kwake   hasa hela  ambayo  hutolewa  kwa  mtindo wa  mwisho  wa  mwezi  au kila  wiki  au  vinginevyo.

Utakapo pokea  hela  kwa  mtindo  huo basi  hadhi  ya  mtu  huyo  itabadilika  na  kuwa  ya  kiupangaji. Lakini  ikiwa  hautaki  awe  na  hadhi  hiyo  basi  si  vema  kupokea hela  kutoka  kwake  kwa  mtindo  huo.   Hii  inahusu  hata  yule  anayempa  mtu  makazi  huku  akimpa  sharti  la  kumlindia  eneo  au  kulihudumia  eneo  na  kuifanya huduma  hiyo  au  ulinzi  huo  kuwa  kama   malipo  yake ya  kumpa  makazi.  Kisheria kwa  kulinda  eneo  ikiwa  kama  huduma  ya  kulipia  makazi  basi  mtu  huyo anakuwa  ni  mpangaji  na  anakuwa na  haki  zote  za  kiupangaji  na  hawezi  kuondolewa  katika  lile  eneo  bila  kuzingatia  haki  zake  kama mpangaji.

2.  SIKU  ZILIZOZIDISHWA  BAADA YA  KODI  KUISHA  INABIDI  KULIPIWA  FIDIA.

Mpangaji  anayezidisha  siku  baada  ya  zile  siku  za  mkataba  kuisha    basi  zile  alizozidisha  inabidi  azilipie  fidia  kisheria.  Kama  mkataba  wake  ulikuwa  unaisha  tarehe  10/10/    na  yeye  akaondoka  tarehe  10/12/  basi  kisheria  ibabidi  alipe  fidia  ya  miezi  miwili  aliyozidisha.  Na  ulipaji  wa  fidia   ya  namna  hii  huwa  ni mara  mbili   katika  muda  aliozidisha. Yaani  kama  kwa  mwezi   alikuwa  akilipa  laki  moja  na  sasa  amezidisha  miezi  miwili  basi   kila  mwezi  aliozidisha ataulipia  mara  mbili  ambayo  ni  laki  mbili  kila  mwezi  na  hivyo  atalipa  laki nne  kwa  kuzidisha  miezi  miwili.  Hivi  ndivyo  fidia  kwa   aliyezidisha  muda  wa   pango  huhesabiwa.

3.     UPANGAJI  WA  UTASHI.

Kwa  jina  la  kitaalam  upangaji  wa  utashi  huitwa  “tenancy  at  will”.  Hii  ni  aina  ya  upangaji  ambapo  mpangaji  na  mwenye  nyumba hukubaliana  kama  ilivyo  kawaida  lakini  kwa  sharti  kuwa  mwenye  nyumba  atasitisha  upangaji  wa  mpangaji   wakati   wowote  atakapoamua.  Upangaji  wa  kawaida  tuliozoea  katika  mkataba  wa  pango  mpangaji  na  mwenye  nyumba  huwekeana  muda  wa  kumalizika  kwa  mkataba  wa  pango  na  mara  nyingi  huwa  ni baada  ya  miezi  sita  au  mwaka  mmoja  na wengine  huwa  ni  zaidi  ya  hapo.  Muda  wa  kuisha  kwa  upangaji  huwa  ni  kitu  muhimu  sana   katika  mikataba  ya  kawaida   ya  upangaji.  

Lakini  hali ni  tofauti  kabisa  katika   mikataba  ya  upangaji  wa  utashi  ambapo muda  huwa  hauwekwi  bayana  ikiwa  na  maana  yeyote  kati  ya  mpangaji  au  mwenye  ardhi  anaweza   kumaliza upangaji  muda  wowote.  Nalieleza hili ili  watu  wasije  kuingia  katika  mtego  kwa kusainishwa mikataba  ya  upangaji  bila kuweka  bayana muda  wa  upangaji.  ifahamike  kuwa  unaposaini mkataba ambao  hauweki  bayana  muda  wa  upangaji    basi   upangaji huo  unageuka  na  kuwa  upangaji  wa  utashi( tenancy at will)   na  ikiwa  wewe  ni  mpangaji  basi  ,mwenye  nyumba ana  haki ya  kukuondoa  katika  nyumba/duka   muda  wowote.

0 comments:

Post a Comment