Pages

Subscribe:

Friday, March 31, 2017

STORY: NILIACHA USISTER NIKAWA MCHAWI 10

Image result for ROMAN CATHOLIC SISTER
Nilimwangalia mama kama kuna hatua nyingine baada ya tukio lile, naye akaniashiria nimchape makofi yule. Nikainua mkono mmoja na kumchapa makofi kwa mbali katika shavu lake la kulia, akashtuka na kujishika shavu hilo huku akifuta kwa mkono kuonesha kwamba ameumia, nikafanya vile tena na mkono wa kushoto, akayumbia kulia kwangu kuonesha kwamba kofi lilimpata. Kisha nikatumia akili zangu sasa, nikaifanya mikono kwa ishara ya kumzungusha, akaanza kuzunguka ndani ya chumba kutoka sehemu moja kwenda nyingine akiwa hajitambui kwa lolote. 

Nikamsimamisha, akasimama wimba huku mikono ameikunjia kifuani. Nilimyooshea mikono sista mwingine pale kitandani, naye akaamka kwanza. Halafu likafuata zoezi la...
kuinuka na kukaa, ndipo likaja zoezi la kutoka kitandani kunifuata nilipo. Sista huyu ni yule ambaye aliwahi kukemea wakati mimi naandamwa na maajabu ya kichawi, kwa hiyo nilikuwa namwogopa kwani niliamini angeweza kunishinda lakini nilipomwona anaamka na kunijia nikasema moyoni hana kitu. Alikuwa anakaribia kuweka mguu wa kwanza chini nikashtuka kumsikia akisema ‘asante Yesu’ kisha mama akanishika kichwani haraka na kufumba na kufumbua tukawa tumesimama nje ya jengo. Mimi nilijiona kawaida lakini mama alikuwa akihema sana. 

“Mama kuna nini kwani?” nilimuuliza kwa sauti ya chini na ya woga. “Mwanangu kuna hatari kubwa.” “Ipi mama, hakuna kifo lakini?” “Kifo hakuna, ila kama ningekuacha, kifo kingetokea.” “Mama turudi nyumbani basi,” nilisema nikianza kuporomosha machozi. 

“Usilie mwanangu, hatari yenyewe imeisha.” Mama alinishika mkono wa kushoto, akanisimamisha wima halafu akasema tuondoke. Kufumba na kufumbua tulikuwa nje ya nyumba yetu, kwa pembeni kuna kibanda cha kuuza chipsi ambapo tulikuta watu wanaendelea kuuza na kununua. Mama aliniambia tusiingie kwanza ndani nyumbani, akatala twende kwenye kibanda kile kuendelea kuwafanyia watu vitendo vya kishirikina. 

Tulipokaribia, mama aliniambia nisimame pembeni kidogo kisha yeye aende kufanya vitendo vya kichawi. Alitaka nijifunze kwa kumwangalia yeye. Mama alipofika, alisimama jirani kabisa na karai lenye mafuta la kukaangia chipsi, akawa anaweka mkono juu ya karai kama mtu anayetaka kuuingiza mkono huo ndani kabisa ya karai. “Mungu, wangu mama anataka kufanya nini tena?” 


nilijiuliza mwenyewe. Nilimwona mama akipeleka mkono juu na kuurudisha chini kwenye karai lakini hakuutia ndani ya mafuta. Akaondoka kwenda kukaa kwenye benchi ambako wateja walikuwa kama watatu tu, alikaa jirani na wateja wawili.

 Alikaa katikati yao halafu akawa anamsogelea mmoja mpaka anakaribia kumgusa kisha anamwacha na kufanya hivyo kwa mwenzake. Alifanya hivyo kama mara tatu. Mama akanifuata mimi na kusimama akiniangalia akaniuliza kama nina swali. “Sasa pale mama faida yake ni nini?” “Nimetengeneza ugomvi mkubwa sana, subiri uone utakavyotokea.” Mama alipomaliza kusema hivyo tu, yule mtu aliyekuwa akikaanga chipsi alimwambia mteja mmoja kwamba jana yake alifika pale akala bila kulipa madai ambayo mteja huyo aliyapinga kwa nguvu zake zote.

Hali hiyo iliibua mzozo mkali kati ya mteja yule na mkaanga chipsi. Mimi niliamini hapo ndiyo wangekuwa wamemaliza, lakini kumbe wao ndiyo wakawa chanzo cha ugomvi mkubwa baina ya yule mteja na mteja mwenzake. Kama nilivyosema mwanzo, mama alikaa katikati ya wateja wawili akawa anawasogelea kila mmoja mpaka karibu sana na kumrudia mwenzake. “Oyaa! Oyaa! Mbona mnanipigia kelele sana?” yule mteja wa pili alisema kwa sauti akipinga mzozo wa wale wengine. 

“Ondoa ujinga wako wewe, nani unamwita oyaa,” alihoji mteja wa kwanza, palepale hali ikabadilika ghafla.Yule mteja wa kwanza alimsukuma mteja wa pili mpaka akaangukia kwenye kindoo cha maji ya kunawa na kukipindua, maji yote yakamwagika. Aliposimama alimrushia konde mwenzake, naye likampata kwenye kichwa, akaanguka chini kama na yeye alivyomwangusha mwenzake kwa kumsukuma sema tu bahati nzuri hapakuwa na kitu pale alipoangukia. 

“Ha! Unaweza kunidharaulisha hivi mimi? Unajua mimi nani?” “Sitaki kujua, haitanisaidia.” “Basi nitakuonesha.” “Hata mimi nakuonesha leo.” Zilipigwa pale, tena ngumi za kwelikweli kiasi kwamba nilianza kuhisi mwenye makosa ni mama ambaye aliinjinia tukio lile la ugomvi. Yule anayekaanga chipsi alishindwa kuzuia, akafunga harakaharaka na kutoka mbio. 

Bahati mbaya sana alisahau kisu kwenye benchi moja, mteja wa kwanza akakiona, akakiokota na kumchoma nacho mwenzake, palepale yule akanyoosha miguu ya kukata roho. “Mama,” niliita. “Nini?” “Si wewe umesababisha.” “Ni moja ya majukumu mwanangu, sasa twende nyumbani maana hata ushetani kwa wale uwatoke.” 

Itaendelea

0 comments:

Post a Comment