Pages

Subscribe:

Friday, March 31, 2017

RIHANNA ATARAJIA KUPOKEA TUZO KUTOKA SHULE HII

Mwanamuziki wa Kike kutoka nchini Marekani Rihanna anatarajia kupokea tuzo kutoka kwenye shule ya mitindo maarufu inayojulikana kwa jina la “The Parsons School of Design”.

Hii ni Tuzo nyingine kwa mwanamuziki huyo, mara baada ya muda mfupi kupokea heshima kubwa ya kutajwa kama Harvard’s Humanitarian of the Year ikiwa ni  heshima ambayo imemweka kwenye ligi moja...
na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan na muigizaji James Earl Jones.
Heshima hiyo kutoka Harvard ilitokana na shughuli zake za kusaidia elimu katika nchi maskini kupitia taasisi yake ya Clara and Lionel Foundation.

Kwa mujibu wa Billboard imeripoti kuwa, Kwa kipindi cha nyuma chuo hicho cha sanaa na ubunifu kilitoa tuzo hiyo kwa Donna Karan ambae ni mwanzilishi wa kampuni inayojihusisha na mitindo DKNY yani, Donna Karan New York.

Imeelezwa kuwa tuzo hiyo ni maalum kwa ajili ya watu ambao wanawawezesha na kuwasaidia wasichana wadogo. Na chuo cha parsons kimempa heshima hiyo Rihanna kutokana na kazi zake za muziki, wanamitindo, na uhisani wake.

Na septemba mwaka huu tutegemee kumuona Rihanna pamoja na kampeni yake ya clara lionel kwenye tamasha la diamond ball kwaajili ya kusaidia kuchaingia fedha za afya na elimu duniani kote.

0 comments:

Post a Comment