Pages

Subscribe:

Wednesday, March 29, 2017

WEUSI WAELEZA MAANA NA JINA LA WIMBO WAO ''YA KULEVYA''



‘Ya Kulevya’ ni moja kati ya majina ya nyimbo zilizowashtua mashabiki hasa katika kipindi hiki tulichopo sasa. Weusi wamefunguka maana ya jina la wimbo huo. 

Akiongea kwa niaba ya wasanii wa kundi hilo, Nick wa Pili amekiambia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, wimbo huo unamuhusu baba anayependwa kwenye familia yake lakini...
baada ya muda upendo huo unamlevya na kuanza kufanya vitu vya tofauti.

“Inamzungumzia baba wa familia kama kiongozi aliyepewa dhamana ya kuiongoza familia, mama na familia imempenda sana baba. Kawaida ya baba akipendwa anachukulia poa, upendo umemlevya baba anaanza kufanya mambo yasiyofaa, anakuwa mtu wa ‘totoz’, Kiki,” amesema Nick.

“Msanii ni zao la mazingira yake tumetumia maneno yanayozunguka sasa hivi tumeyatoa kwenye ‘muktadha’ yake tumeyaleta kwenye wimbo wetu tukatoa kitu,” ameongeza.

0 comments:

Post a Comment