Pages

Subscribe:

Friday, March 31, 2017

DIAMOND PLATNUMZ AELEZA A-Z ANAVYOPATA UTAJIRI

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’, amefichua moja ya siri ya mafanikio yake makubwa kiuchumi ni kusaidia watu wenye uhitaji.

Diamond ambaye anatajwa kama msanii anayeongoza kwa kipato nchini, amesema anajisikia ufahari mkubwa kuona anaweza kuwasaidia watu wenye uhitaji na amekuwa akipata... baraka zaidi kupitia kazi zake.

“Unajua watu wengi hawajui ukitoa unazidi kubarikiwa, hii kwangu imekuwa sehemu ya mafanikio sana, huwa najisikia mwenye bahati kubwa nikimsaidia mtu mwenye uhitaji kwani naamini lazima nitafanikiwa,” alisema Diamond.

Alisema amekuwa akikutana na changamoto nyingi ikiwamo watu wengi kuhitaji msaada kutoka kwake, lakini amekuwa akiwalenga wale ambao yeye anaamini wanahitaji msaada zaidi kwake.

0 comments:

Post a Comment