Pages

Subscribe:

Wednesday, March 29, 2017

KAULI YA WEUSI JUU YA KOLABO YAO NA BELLA



Mwaka jana, collabo ya kundi la Weusi na Christian Bella ilivuja lakini ikaja kubainika kuwa wameingia tena studio kuifanya upya na kuiboresha zaidi ili kuiachia rasmi.  Hata hivyo, Weusi wameonesha kuiweka benchi bado ngoma hiyo baada ya wiki hii kuachia wimbo mwingine, Ya Kulevya. 

Nick wa Pili ameelezea hatma ya collabo hiyo:
“Kazi ya Bella tuliirudia upya, ni kazi kali, ni project kubwa itakuja muda wake ukifika na tunataka tukitoa, tutoe...
audio na video kwa pamoja,” rapper huyo alikiambia kipindi cha Extra Fleva cha Uplands FM kinachoendeshwa na Ergon Elly.

Kwa upande wa video ya Ya Kulevya, Nick amesema haitachukua muda mrefu kuanza kuonekana kwenye TV.

0 comments:

Post a Comment