Pages

Subscribe:

Wednesday, March 29, 2017

ISHUNYA BARAKAH KUHAMA ROCK STAR 400 KURUDI KWENYE LEBO YAKE YA ZAMANI MWENYEWE AFUNGUKA


Kitaani kuna tetesi kumuhusu hitmaker wa ngoma ya Acha Niende Baraka Da Prince kutaka kuondoka katika uongozi wa lebo ambayo inamsimamia kwasasa inayofahamika kama Rock Star 4000 na kurudi kwenye uongozi wake wa zamani wa mtu mzima Mgalula Fundikila.

Mwandishi ameona sio kesi kama itacheza nje ya box na story hizo na kumtafuta muhusika mkuu ambaye ni Baraka Da Prince na kupiga nae story kuhusiana na ukweli wa tetesi hizo na yeye kufunguka...


“Sio kweli, hata nyimbo yangu mpya nadhani wanaisimamia Rockstar, album yangu wanaisimamia Rockstar na hata projects zangu zote wanasimamia Rockstar, bado nipo chini ya Rockstar na tunafanya kazi na wala hakujawahi kutokea mtafaruku wowote kati yangu na hawa jamaa. Sijawahi kumpigia Mgalula na wala kuongea nae chochote kuhusiana na kufanya nae kazi.” Alisema Baraka Da Prince.

Pia Baraka alizifananisha tetesi hizo na mtu ambaye amejenga ghorofa halafu anataka kulibomoa ili ajenge nyumba ya kawaida, na kudai kwamba mtu huyo atakuwa hana akili timamu.
Story kamili ipo kwenye video hii hapa chini, bonyeza play uweze kumsikiliza Baraka Da Prince akifunguka mwanzo hadi mwisho.

0 comments:

Post a Comment