Pages

Subscribe:

Tuesday, March 28, 2017

BILL NASS: SINA MAHUSIANO NA MWANAMKE YEYOTE NA SIFIKIRII KUOA



Je unajua sababu inayomfanya Bill Nass awe msiri katika mahusiano yake? Rapper huyo amefunguka sababu inayomfanya awe hivyo. Akiongea na kipindi cha Bongo Dot Com cha Times FM, hitmaker huyo wa Mazoea amesema alishawahi kuwa katika mahusiano mengi ambayo ambayo hakuwa na bahati nayo.

“Nimekuwa kwenye mahusiano mengi ambayo sikuwa na bahati nayo pia inaweza kukutengeneza kisaikolojia kutokana na mambo ambayo nayaona kwa...
rafiki zangu. Nina bahati ya kuona hivyo vitu kwa hiyo sijui huko mbele mahusiano ni suala la feelings,” amesema rapper huyo.

Bill ameongeza kwa sasa hana mahusiao na mrembo yoyote wala hajawahi kufikiria kuoa hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment