Pages

Subscribe:

Thursday, March 30, 2017

STORY: NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE-23

Image result for nilifanya mapenzi na maiti 20 ILI NITAJIRIKE-21

ILIPOISHIA
Nilitoka kijijini kwenda Dar kutafuta utajiri kwani maisha ya kimaskini niliyoishi yaliniumiza sana. Nilipofika huko, nikakutana na mtu aliyeniambia niende kwa mganga fulani ambaye ndiye aliyeniambia nifanye mapenzi na maiti ishirini. Tayari nimefanya na kumi na tisa mochwari, sasa bado hii moja ambayo imesimama nyuma yangu makaburini tulipokuwa.


SONGA NAYO
Nliuliza swali hilo huku nikitetemeka sana, nilitamani nipotee na kutokea sehemu tofauti na hiyo. Mwili haukuacha kusisimka, kuna kipindi niliyasikia...

kabisa mapigo ya moyo yalivyokuwa yakidunda kwa nguvu.

“Mimi ni mpenzi wako uliyemfuata hapa makaburini, una ngozi laini sana, hakika wewe ni mwanamke wa ndoto yangu,” niliendelea kuisikia sauti hiyo.
Mara mguso wa mtu huyo ukahama kutoka begani mwangu na kuanza kuelekea chini, nilizidi kutetemeka mno, mikono yake ikahamia katika mgongo wangu na kuanza kuushikashika, baadaye akahamia katika kiuno changu, nikabaki nikianza kulegea mwili wangu.


“Ni kipindi kirefu kimepita, miaka kumi pasipo kumgusa mwanamke yeyote yule, upo tayari mpenzi wangu?” aliniuliza.
Sikumjibu, nilibaki kimya, wakati nikiwa nimesimama vilevile, ghafla nikaanza kuona mazingira ya mahali pale yakianza kuondoka na mazingira mengine kuingia.


Mbele yangu kukaonekana kuwa na kitanda kikubwa, ndani ya chumba kikubwa, alichonifanya ni kunisukumia kitandani, niliona kweli nimeangukia kitandani, ila ukweli ni kwamba niliangukia ndani ya kaburi lake, kitanda, lilikuwa jeneza lake, alichokifanya, naye akaja kwa juu yangu mgongoni, nikajigeuza ili nimuone, sikumuona, ila miguso yake, ilionesha alikuwa hapo pamoja nami kwani yeye ndiye alianza kunivua nguo, yaani nalivuliwa nguo na mtu nisiyemuona.


Nilitakiwa kutulia vilevile, kumbuka kwamba nilifanya mapenzi na maiti kumi na tisa na hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho, hivyo niliona kuwa na sababu zote za kutulia kwani baada ya hapo, nilikuwa na uhakika wa kupata utajiri kama alivyoniambia mganga yule.


Ndani ya kaburi lile ndipo tulipoanza kufanya mapenzi, maiti ile ilikuwa ikinuka sana, sikuwa nikiiona ila niliihisi miguso yake kila kona katika mwili wangu.
Nilifanya naye mapenzi kwa saa moja ndipo akamaliza, nikahisi akiondoka mahali hapo na kuisikia sauti ya mganga ikinipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanya, sasa ningekuwa tajiri mkubwa.


“Umefanikiwa, sasa utakuwa tajiri mkubwa tu,” nilisikia sauti ya mganga.

Nilichokifanya ni kutoka nje ya kaburi na kuvaa nguo zangu. Kilichonishangaza, ghafla nikaanza kuona moshi mzito ukifuka kutoka ndani ya kaburi lile, sikujua nini kiliendelea, moshi ule mzito ukalifunika kaburi lote hata lisionekane, wakati nashangaa ghafla moshi ule ukakatika na kaburi lile kujifukia kama lilivyokuwa mwanzo.

Sikutaka kubaki mahali hapo, nikatoka na kuelekea nje ya eneo la kaburi lile huku tayari ikiwa ni saa nane usiku. Nilimkuta mganga akiwa amekaa pembeni akinisubiri, aliponiona, kwanza akatoa tabasamu pana, nikamsogelea.
“Hongera sana, hakika umenifanya nijisikie fahari sana,” aliniambia mganga yule.
“Kwa hiyo lini nitapata utajiri?”
“Utaanza kesho, ila nataka ufanye kitu.”
“Kitu gani?”
“Biashara yoyote ile…”
“Mmh!”
“Ndiyo hivyo! Utakapoanza, amini kwamba ndipo utajiri utakapoanzia,” aliniambia huku akinikazia macho.


Nilichokiamini ni kwamba mara baada ya kufanikiwa kufanya mapenzi na maiti zile basi ningepata utajiri kwa kukuta begi la fedha likiwa sehemu kumbe sivyo.

Akaniambia natakiwa kufanya biashara ambayo ndiyo ingekuwa chanzo cha utajiri wangu, sikuwa na jinsi, japo kwa shingo upande, nikakubaliana naye. Na hivyo kuondoka mahali hapo.

Siku iliyofuata, nikamwambia Dickson pale Ubungo kwamba nilitaka kufanya biashara na biashara yenyewe ambayo niliichagua ilikuwa ni kuuza magazeti, akanikubalia hivyo kutafuta meza na kuanza kufanya harakati zote za kuhakikisha magazeti yanauzwa mara moja.


Siku mbili zilizofuata, tayari nilikuwa na meza yangu, niliweka juu magazeti mengi, nikatafuta vitabu vya hadithi na kutulia. Kitu cha ajabu ambacho sikuwahi kukiona ni pale watu walipoanza kumiminika katika meza yangu na kuanza kununua magazeti.

Nilishangaa, huwa ni vigumu kwa magazeti kumalizika kwa saa moja, lakini huwezi kuamini, magazeti mia moja niliyopewa, yote yaliishia ndani ya saa moja tu. Si mimi niliyeshangaa, hata watu wengine wa pale walishangaa pia.

Haikuwa kawaida kabisa na sidhani kama iliwahi kutokea. Magazeti yakaisha lakini nikashangaa watu wengine wakija mezani kwangu, waliiona meza ikiwa tupu ila wakawa wananiuliza kuhusu magazeti, yapo au yamekwisha, nilishangaa, meza ilikuwa tupu, sehemu zingine zilikuwa na magazeti, kwa nini hawakwenda huko?
Huo ulikuwa mwanzo, niliendelea kufanya biashara ya kuuza magazeti, ikaanza kuyabadilisha maisha yangu, nikawa naongezewa magazeti mengi, nikaanza kuyaona maisha yakianza kubadilika, fedha ziliingia, baadaye nikaanzisha biashara nyingine ya kuuza juisi na maji, hiyo ndiyo iliyoniingizia fedha zaidi na hivyo kupanga chumba Manzese Midizini.

Naweza kusema huo ulikuwa mwanzo tu, ndani ya miezi mitatu tangu nianze kufanya biashara hizo, nikashangaa nikiwa na akiba ya milioni tatu chumbani kwangu. Sikujua nilizipataje, ila nilichokijua ni kwamba kulikuwa na nguvu fulani nyuma yangu, nikafanikiwa zaidi.
Ulipoingia mwezi wa tano tangu nifanye biashara hizo, nikajikuta nikiwa na milioni tano. Nikashtuka, utajiri ukaanza kuninyemelea pasipo kukumbuka kwamba unapokuwa na utajiri wa kishetani huwa huna furaha, huna amani ni utajiri unaotesa na kuumiza mno. Huo ndiyo ukaanza kuninyemelea. Mara ya kwanza, sikujali, ila baadaye, nilikuja kujuta kwa nini nilitaka utajiri.
Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment