Pages

Subscribe:

Thursday, August 31, 2017

CHEGE WIMBO WANGU NA CHID BENZ UTAKUWA NAMBA MOJA KWENYE ALBAM



Msanii wa Bongo Flava, Chege ameeleza kuwa albamu yake imeshakamilika huku akitolea ufafanuzi ngoma yake na Chid Benz.

Chege amesema albamu ni kitu kikubwa sana ambacho msanii hapaswi kukurupuka, hivyo amejipanga kiasi kwamba kila wimbo ulio...
ndani anaweza kuutoa na watu wakaelewa.

“Albamu itakuwa na ngoma 12 au 15 kwa sababu nimetengeneza ngoma kama 17, ni mimi tu na watu wangu kupanga hapa tuweke ngapi kwa sababu zimekamilika zote tayari,” Chege amedai

“Na hiyo ngoma unasema na Chid Benz ndio ngoma ambayo nafikiri itakuwa namba moja kwenye albamu yangu, ngoma hiyo imeshafanyiwa mixing na ilikuwa itoke ni vitu vikawa vimeingiliana tukoana tuiweke kwenye albamu watu wataisikia katika mtindo mwingine,” ameongeza.

Pia amesema ni ngoma chache sana amefanya pekee yake kwani ngoma nyingi amefanya kwa mtindo wa kolabo na wasanii wa Nigeria, Afrika Kusini n.k.

0 comments:

Post a Comment