Pages

Subscribe:

Thursday, August 31, 2017

THAILAND MWANAMKE KABLA YA KUOLEWA ANATAKIWA AKASOME KOZI HII KWANZA


Kuolewa au kuoa mtu kutoka Taifa lingine ni jambo la kawaida na mara nyingi inapotokea hivyo kuna vigezo vya kawaida tu ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za nchi husika lakini zipo nchi nyingie jambo hilo si rahisi kama kulitaja tu kinywani.

Unaambiwa katika nchi ya Thailand kumeanzishwa utaratibu maalumu wa kutoa kozi ya bure kufundisha wanawake wazawa wa nchi hiyo namna ya...
kumudu ndoa zao endapo watabahatika kuolewa na wanaume wa mataifa mengine duniani.

Kama ilivyo sehemu nyingi duniani, wanawake wa Thailand pia huamini kuolewa na mwanaume wa Taifa la mbali hasa Marekani na Ulaya ni njia ya kujikwamua kiuchumi na kuwa na maisha bora.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii ya Thailand imeeleza kuwa kozi hiyo imejikita katika kuwafundisha jinsi ya kufanya mambo mbalimbali katika nchi watakazoolewa, sheria za nchi hizo, jinsi ya kujiandaa kabla ya kwenda na mengineyo.

0 comments:

Post a Comment