Pages

Subscribe:

Thursday, August 31, 2017

NIYONZIMA: NAWEZA KUPENDA AU KUPENDWA ILA KABULA SIYO TYPE YANGU

Mchezaji wa klabu ya Simba Haruna Niyonzima amefunguka na kusema kwamba muigizaji Miriam Jolwa, Kabula  aliyewahi kutangaza ana mahusiano naye na kwamba hafahamu kwa nini mwanamke huyo aliamua kumchafua  huku akidai siyo 'type' yake.

Niyonzima amedai kuwa wakati Kabula anaongea maneno hayo hakuwepo ndani ya nchi lakini pia aliogopa maneno hayo kwani yalimuharibia kwenye...
familia yake huku akizingatia kwamba tayari yeye ni baba ni wa familia.

"Mimi ni binadamu naweza kupenda au kupendwa lakini Kabula hakuwa 'type' yangu. Nilimchukulia kama msichana wa ajabu. Mke wangu angekuwa siyo muelewa basi angekuwa ameshaniacha. Mke wangu hakupenda kile kitu ukizingatia mimi nimetoka huko kwetu na mke wangu, aliumia sana ingawa anajua mimi siyo mtu wa kufanya vitu kama hivyo," Niyonzima

Ameongeza kuwa "Kwa mwanamke ambaye anajielewa asingeweza kutangaza mbele za watu kama anatembea na mtu hata kama ni kweli  lakini siyo sahihi" 

Akizungumzia kuhusu kwenda kumuona muigizaji huyo hospitali baada ya kupata matatizo ya kuugua, Niyonzima amesema "Ukweli mimi ni Muislam namuombea Mungu amsaide lakini siwezi kwenda kumuona kwa kitendo alichokifanya cha kunichafua sitaweza. Mimi siyo pretender"  alisisitiza

0 comments:

Post a Comment