Pages

Subscribe:

Tuesday, August 29, 2017

HII NDIYO SABABU ILIYO PELEKEA DUKA LA JUX KUVUNJWA

Msanii Jux ambaye ni mmiliki wa duka linalo uza nguo za 'brand' yake ya 'African Boy', ametoa sababu iliyofanywa duka hilo lipitiwe na bomoa bomoa, katika eneo la Sinza jijini Dar es salaam. 

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Jux amesema duka hilo limevunjwa kwa sababu mwenye nyumba alikuwa na...
mgogoro na Mahakama kuhusu kiwanja hicho ndipo Mahakama ilipoamuru nyumba hiyo ivunjwe japo hawakupewa taarifa ya aina yoyote na mwenye nyumba huyo.

Nimepata hasara kubwa kwa kuvunjwa kwa jengo hilo kwa kuwa kuna baadhi ya vitu vimepotea pamoja na pesa taslimu shilingi Milioni moja imeibiwa na mpaka sasa, baba mwenye nyumba wangu hapatikani na sijui yupo wapi ?", alisema Jux

0 comments:

Post a Comment