Pages

Subscribe:

Tuesday, August 29, 2017

MR BLUE: MUNGU AMENIFANYIA MAMBO MAKUBWA

Msanii Mr. Blue ametoa sababu iliyomfanya kuingia studio na kuimba wimbo wenye kumtukuza Mungu tofauti na wengi walivyo mzoea, na kusema kuwa alifanya hivyo kwa mapenzi yake na shukrani kwa Mungu. 

Akizungumza na mwandishi wetu Mr. Blue amesema kuwa siku zote amekuwa akitumia sanaa yake kufurahisha watu kwenye starehe, lakini...
Mungu amemfanyia mambo makubwa ambayo hakuwahi kufikiria angeweza kuyafanya maishani mwake, hivyo akaona ni vyema kuandika wimbo wa kumshukuru.

“Nimeshika peni kuandika ile nyimbo kutokana na kuona Mungu amenibariki kama kijana, nimetembea dunia nzima, nimefanya vitu ambavyo sikuwahi kuviweza kama mtoto wa kimasikini, hiyo ndio sababu kubwa, kutoa shukurani kwa Mungu kwa aliyonifanyia”, alisema Mr. Blue.

Hivi karibuni Mr. Blue aliwashangaza mashabiki wake kwa kuimba wimbo wenye kumsifu Mungu, tofauti na vile alivyozoeleka tangu alipoanza muziki huu wa bongo fleva.

0 comments:

Post a Comment