Pages

Subscribe:

Monday, August 28, 2017

MRISHO MPOTO AFUNGUKA SIRI YA VIJANA KUSHINDWA KUMUDU MAPENZI

Msanii wa muziki wa mashairi Tanzania Mrisho Mpoto, amefunguka kuwa wasanii wengi wa sasa hivi wanaoimba nyimbo za mapenzi hawayajui mapenzi, ndio maana nyimbo hizo hazikai kwa muda mrefu. 

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Television, Mrisho Mpoto amesema mapenzi ni kitu kigumu na ndio maana...
vijana wengi yanawashinda, lakini ipo siku na yeye atakuja kuimba wimbo wa mapenzi na kuwashangaza mashabiki, kwani yuko vizuri kwenye sekta hiyo.

"Ndio maana ndoa zao hazikai mapezi magumu kaka , hawa wasanii wetu wanaimba mapenzi mapenzi yao hayakai, mi nitakuja kuimba mapenzi utasema huyu jamaa alikuwa wapi sikuzote, nitakuja kuimba mapenzi ambayo mtu akisikiliza atasema kweli Mpoto kazungumzia mapenzi, vijana mapenzi hawajui", alisema Mrisho Mpoto

Kutokana na kauli hiyo Mrisho Mpoto ameweka wazi kuwa anatarajia kuachia wimbo akiwa na Kassim Mganga, wenye ujumbe wa mapenzi na atashangaza mashabiki kwa watakachosikia.

0 comments:

Post a Comment