Pages

Subscribe:

Tuesday, August 29, 2017

NYASHINSKI AIKUBALI NYIMBO MPYA YA JUX NA KUSEMA HAYA

Rapa Nyashinski kutoka nchini Kenya ambaye sasa anafanya vyema na ngoma yake 'Aminia' amefunguka na kunyoosha mikono kwa msanii wa bongo fleva Jux African Boy ambaye sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya 'Utaniua'. 

Nyashinski alishindwa kuzuia hisia zake juu ya wimbo huo mpya wa Jux na kusema ni moja ya wimbo mzuri na mkubwa ambao huwezi...
kujutia muda wako kuusikiliza na kuutazama kutokana na uzuri wake.

Mbali na hilo Nyashinski amempa pongezi muongozaji wa video kutoka Tanzania Hanscana kwa kazi nzuri na kusema katika wimbo wa Jux ameutendea haki sana kwani video yake ni kali mno pia. 

Jux alishawahi kukiri kuwa wimbo huo aliutunga rasmi kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee ambaye kwa sasa inasemekana wamekosana na kudai kuwa japo alimuimbia Vanessa lakini kitu alichoimba kwenye wimbo huo ni kitu ambacho kinaweza kumkuta mtu yoyote yule kwani matukio hayo yapo kwenye jamii na yanatokea kila siku kwa wapenzi kuachana pasipokuwa na sababu ya msingi na kuumizana.

0 comments:

Post a Comment