Pages

Subscribe:

Sunday, August 27, 2017

OMMY DIMPOZ AAMUA KUICHOKOZA TIMU NZIMA YA WCB



Baada ya Ommy Dimpoz wiki hii kuandika ujumbe ambao uliichafua team nzima ya WCB na baadaye kuufuta, mkali huyo wa wimbo Cheche, Jumamosi hii amepost tena na kuufuta ujumbe mwingine ambao unaodaiwa kuwa ni dongo kwa WCB ambao wameachia wimbo mpya ‘Zilipendwa’.

Wadau wa mambo wamedai Ommy Dimpoz ametuma ujumbe huo baada ya WCB kuachia wimbo mpya muda mchache baada ya...
mpinzani wao mkuu, Alikiba kuachia wimbo, Seduce Me ambao mpaka sasa unaongoza kupitia mtandao ya YouTube.

Muimbaji huyo wa RockStar4000 alipost picha ya tembo mtandaoni akimaanisha Alikiba akiwa amezungukwa na simba wengi ambao wanadaiwa kuwa ni team ya WCB

Picha hiyo alikuwa na ujumbe, “Watoto Wangu eeeh!! eeehh!! Mimi Baba Yenu eeeeh!! Sina Nguvu tenaaa Eeeeh za kuua Tembooo.

Watoto: Sawa Baba tunakuja kukusaidia Sema itabidi tutumie zilezile mbinu zetu za UJANJA UJANJA si Unajua sikuhizi hayuko peke yake kuna mwingine kajificha”
Ujumbe huo umetafsiriwa na wadau wa mambo kwamba Diamond alishindwa kupambana na Alikiba peke yake ndipo alipoamua kuachia wimbo akiwa na wasanii wake (WCB) ili kupamba na muimbaji wa RockStar4000.

0 comments:

Post a Comment