Pages

Subscribe:

Wednesday, August 30, 2017

DIAMOND, LULU NA ALIKIBA WATAJWA KWENYE ORODHA YA HAWA WATU 100 AFRICA



Mastaa wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Alikiba na Diamond Platnumz wametajwa kwenye orodha ya vijana 100 waliochini ya miaka 40 wenye ushawishi zaidi barani Africa kwa mwaka 2017.

Kwenye orodha hiyo iliyotolewa leo na mtandao wa African Youth Awards imemtaja pia muigizaji wa filamu nchini Tanzania mrembo Elizabeth ‘Lulu’ Michael na mwanamitindo...
Flaviana Matata kwenye orodha hiyo ya vijana 100 wenye ushawishi zaidi barani Africa.



Wengine waliofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo ni Miss Tanzania 2005 na Mjasiriamali, Nancy Sumari, Jokate na mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds FM, Millard Ayo.

Kwa upande mwingine wasanii waliochaguliwa kwenye orodha hiyo kutoka nje ya Tanzania ni Davido kutoka Nigeria , Rapa AKA kutoka Afrika Kusini na wengine wengi.
Dirisha la kupendekeza majina ya vijana wenye ushawishi zaidi barani Afrika mwaka 2017 lilifunguliwa mwezi June 25 na kufungwa agosti 22 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment