Pages

Subscribe:

Friday, August 25, 2017

NUH MZIWANDA: BAO LA USHINDI NI USHINDI WA KILA KITU



Msanii wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda ametoa maana kamili ya ngoma yake mpya ‘Bao la Ushindi’. Bao la Ushindi ni ngoma ya kwanza kwa Nuh Mziwanda tangu alipaochana na mkewe hivi karibuni. 

Akizungumza na Dj Show ya Radio One Nuh amesema ngoma hiyo inazungumzia mafanikio anayoyapata mtu katika...
utafutaji wake wa kila siku.

“Hii ngoma bao la ushindi nime-produce mwenyewe ni wimbo fulani hivi hauhusiani na mapenzi bali ni ushindi. Mtu unaposema bado la ushindi ujue ni ushindi ule refa anapiga filimbi mpira umeisha,” amesema na kuongeza.

“Ni ushindi wa kila kitu kwenye maisha, ni ushindi wa kila kitu kupata pesa, kupata dili, ku-enjoy na washikaji kama mimi naweza kuzungumzia kupata mtoto na mtu yeyote anaweza akasikiliza,” amesisitiza.

0 comments:

Post a Comment