Pages

Subscribe:

Tuesday, August 29, 2017

TIMBULO BIG UP KING KIBA MIMI SIYO TEAM MOND WALA KIBA


Bado mpambano mkali unaendelea kupitia mtandao wa YouTube, kati ya video ya ‘Seduce Me’ya Alikiba na’Zilipendwa’ ya WCB, huku msanii wa Bongo Flava Timbulo akiibuka na kutoa somo.

Timbulo, ambaye anahit na ngoma ya Mshumaa ameandika katika mtandao wa Instagram kuwa, wasanii wajifunze kupeana nafasi ya...
kutoa ngoma kwani kila mtu anauwezo wake.
“Umefika wakati sasa tujifunze kupeana nafasi na kuamini kuwa kila mtu nafasi alonayo ni mungu amemuweka hapo, haya mambo yakutoa nyimbo kisa fulan katoa unaeza kuta mnaimsaidia mtu promo,
Tembea na hii:- Maandiko yanasema “anaejikweza atashushwa bali yule anayejishusha atakwezwa”
Like kama umma ungenyamaza kwa hili bac mawe yangepaza sauti!
Big up king kiba @officialalikiba #seduceme is a smash hit Nb:Sipo #Ukawa wala #Ccm.”
ameandika Timbulo.
Kauli ya Timbulo imekuja baada ya Alikiba na Diamond, kutoa ngoma kwa wakati mmoja na kufanya baadhi ya ngoma za wasanii wengine waliotoa ngoma kwa sasa kutopata nafasi kwa mashabiki.

0 comments:

Post a Comment