Pages

Subscribe:

Thursday, August 31, 2017

DAX: SIANGALII UKUBWA WA JNA LA MWANAMKE WA KUTOKA NAYE

Mwanamitindo wa kiume ambaye anafanya vizuri kwenye ulimwengu wa mitindo Dax Cruz, ameweka wazi vigezo vya mwanamke ambaye anaweza kuwa naye kwenye mahusiano, huku akiweza wazi hajali kama ni maarufu ama la. 

Akizungumza na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Dax amesema kigezo kikubwa na ngao yake anapotaka kuingia kwenye mahusiano ni...
maelewano baina yake na huyo mtu, na siyo ukubwa wa jina alilonalo kama ni maarufu ama la.

"Kikubwa mimi huwa siwi na mtu kutokana na ukubwa wa jina lake, ndiyo ngao kubwa ya mahusiano yangu, nakuwa na mtu ambaye nimemuelewa na tumeelewana, majina makubwa au umaarufu wake mi huwa sifuati sana”, alisema Dax Cruz

0 comments:

Post a Comment