Pages

Subscribe:

Monday, August 28, 2017

MAN WALTER: WASANII WANAO SHINDANA NA SEDUCE ME YA KIBA WAMEPOTEA

Man Water amebainisha hayo baada ya kuwepo ushindani mkubwa kwa mashabiki mbalimbali na baadhi ya wasanii wakiufananisha wimbo huo wa Alikiba na wasanii wengine huku baadhi yao wakijaribu mpaka kutoa wimbo mpya ili kuweka ushindani baina yao.
"Nyimbo nyingine ambazo zinatoka kwa sababu ya 'audio' hii labda wanataka kujaribu kushindana nayo, mimi naita ni povu. Ni sawa na mtu ana mahusiano na mpenzi wake...
wakaachana halafu 'faster' akaonyesha mahusiano yake mengine mapya kwa watu, 'at the same time' lazima itakuwa siyo mahusiano ya kudumu hayo", alisema Man Water.
Pamoja na hayo Man Water ameendelea kwa kusema "Kiba amejipanga ndiyo maana akatoa ngoma, kama una malengo ya kushindana na 'seduce me' umepotea kwa sababu utakuwa ujatulia na kwa vyovyote vile utakuwa umekurupuka katika ufanyaji wako wa kazi na wimbo hautakuwa na mashiko kuanzia title na life time itakuwa ndogo sana hewani", alisisitiza Man Water.

0 comments:

Post a Comment