Rais wa Manzese, Madee amefunguka kwa kumuomba radhi msanii wa bongo
movie Jacqueline Wolper kwa kitendo cha kumfanya katuni mrembo huyo
katika video yake mpya ya wimbo 'Sikila' bila ya ridhaa yake mwenyewe.
Madee
ameomba msamaha huo mbele ya kamera za eNewz kutokea EATV baada ya
Wolper kudai ataenda kumshtaki kwa kitendo cha kumtumia...
katika kazi
zake bila ya kuwa na makubaliano baina yao kwa kuwa ni kinyume na
taratibu zake.
"Niliamua kumtumia
Jacqueline Wolper baada ya 'director' kuniambia nitafugte picha ya
msanii yeyote maarufu ndipo nikaamua kumpatia picha ya ya Wolper na
kabla ya kumtumia nilimpigia simu, nikampa taarifa ili aelewe
kinachoendelea", alisema Madee.
Pamoja na hayo, Madee amedai haamini kama ni kweli mrembo huyo anataka kumfungulia kesi juu ya jambo hilo.
0 comments:
Post a Comment