Pages

Subscribe:

Tuesday, August 15, 2017

MWANA FA: SIJAWAHI KUOMBA KAZI



Licha ya kwenda shule vilivyo rapper Mwana FA ameeleza ni kwanini hajafikiria kuajiriwa.

“Sijawahi ku-apply (kuomba kazi) kusema kweli nafikiri namna kwenda kazini saa 12 asubuhi na kutoka saa 11 inanipa wakati mgumu. Sisi tunasoma kwa ajili ya...
unajaribu kupanua ubongo wako ili uweze kumudu mazingira yako ya kila siku ama ukitaka kufanya kazi zako uzifanye kwa ule upeo umeupata shuleni”.

Mwana FA alisema hayo katika mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times FM ambapo alieleza kuwa watu wamekuwa na dhana tofauti kuhusu vyeti kwamba ukiwa navyo ni lazima uajiriwe.

“Sasa sisi tunasoma kwa sababu uje na vyeti uajiriwe, siyo usahihi wa watu kwenda shule, kwa hiyo mimi natumia vyeti vyangu lakini sivitumii kwenda kumfanyia kazi mtu yeyote, sivi-apply kwenye muziki, navi-apply kwenye biashara zangu nyingine,” amesema Mwana FA.

0 comments:

Post a Comment