Pages

Subscribe:

Thursday, August 17, 2017

NIKI WA II: SIKU HIZI MTU ANAFANYA MUZIKI ILI APATE UMAARUFU

Msanii Niki wa Pili amewachana wasanii ambao wanatoa kazi ambazo hazina ubora, na kusema kuwa wanaharibu ubora wa muziki wa bongo fleva. 

Akizungumza na mwandishi, Niki wa Pili amesema wakati wao wanaanza muziki walikuwa na kiu kubwa ya kuwa wana muziki, tofauti na wasanii wa wanaoanza kutoka sasa, kwani wanafanya muziki ili...
kuwa maarufu tu, bila kuzingatia ubora wa kazi.

"Sisi wakati tunaanza muziki tulikuwa tunapenda kuwa wana muziki, siku hizi mtu anafanya muziki ili atoke awe maarufu, kwa hiyo kiu yake sio kuwa mwanamuziki mkali, kiu yake ni kutoka, kwa hiyo ukituangalia kurudi nyuma unatukuta tumetengeneza miziki mingi mizuri", alisema Niki wa Pili.

0 comments:

Post a Comment