Pages

Subscribe:

Friday, October 16, 2015

CHRISTIAN BELLA AFUNGUKA PESA ALIZO TUNZWA KWENYE FAINALI YA BONGO STAR SEARCH

Christian Bella amesema show yake ya fainali ya Bongo Star Search Ijumaa iliyopita, ilimuingiza fedha za kutunzwa nyingi zaidi kuliko show zote alizowahi kufanya.
Bella ameiambia Bongo5 kuwa ni mara yake ya kwanza kutunzwa zaidi ya shilingi milioni... 3 na hivyo anawashukuru watanzania kwa upendo wanaomwonyesha.

“Unajua mimi nimekuwa nikitunzwa pesa nyingi lakini haikuwahi kufika kiasi kile. Nakumbuka katika uzinduzi wa wimbo wangu ‘Nashindwa’ nilitunzwa milioni 2, lakini ile ya BSS ndio imevunja rekodi, milioni 3 na laki mbili ni nyingi sana. Nawashukuru sana watanzania. Hii inaonyesha wanakubali ninachokifanya,” alisema Bella.

0 comments:

Post a Comment