Pages

Subscribe:

Thursday, October 15, 2015

MAGUFULI AMPA SIFA DIAMOND BAADA YA KUTWAA TUZO ZA AFRIMMA

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amemmwagia sifa lukuki, mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi iliyopita nchini Marekani.

Tukio hili lilitokea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili mkoani Lindi baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba (Alikiba) kushuka jukwaani kukamua kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais, ndipo Magufuli alishika kipaza sauti na kumsifia Diamond kwa kusema...

“Ukweli nampongeza sana msanii Diamond kwa jinsi anavyojituma na kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu…,” alisema Magufuli huku pia akiwapongeza Ommy Dimpoz na Vanesa Mdee walioshinda tuzo tofauti katika kinyang’anyiro hicho.

0 comments:

Post a Comment