Pages

Subscribe:

Saturday, October 24, 2015

JOKATE: UMAARUFU UNAPOTEZA WASANII WENGI HAPA BONGO

Mwanamitindo na muimbaji, Jokate mwengeleo aka Kidoti ametaka wasanii kutotumia vibaya umaarufu  wao ili wapate ushirikiano katika kazi zao.
Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Jokate amesema

kinachowaponza wasanii wengi ni umaarufu: “Unajua ukiwa maarufu kila mtu akawa anaimba nyimbo yako, ni rahisi kuvimba kichwa ukajiona wewe ndio wewe, unasahau kabla ya wewe kulikuwa kuna...
watu ambao walihit vilevile. Hii ni cycle kwamba leo umehit, yule kesho,” alisema Jokate
“Wanatakiwa kujua sio kwamba wao watakaa juu milele, hiyo haipo. Kwahiyo hivyo vitu visikuingie kichwani, cha muhimu ni kufanya kazi kwa heshima hasa hasa kwa wale watu ambao wapo kwenye industry,” alisisitiza Jokate.

0 comments:

Post a Comment