Pages

Subscribe:

Sunday, October 4, 2015

HAMISA MABETO: NDOA YANGU ITAZINDULIWA MTANDAONI

Imelda Mtema Mwanamitindo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ amefunguka kuwa siku atakayofunga ndoa atafanya siri na watu wataiona kwa mara ya kwanza kupitia mitandao ya kijamii. Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Hamisa alisema kuwa ndoa yake itakuwa ya siri kwa maana atafunga na mumewe Kiislamu bila kuita watu na... picha za ndoa hiyo zitazinduliwa mtandaoni. “Watu wakishaziona picha hizo kupitia mitandao ya kijamii ndiyo nitafanya pati ya kusherehekea, nataka kwangu kiwe kitu cha tofauti kidogo,” alisema Hamisa ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

0 comments:

Post a Comment