Pages

Subscribe:

Saturday, October 24, 2015

MASOGANGE AFUNGUKA BAADA YA TEKNO KUMKANA

masogange
Video vixen wa Bongo, Agness Masogange ameonesha kupingana na kauli ya msanii wa Nigeria, Tekno Miles ambaye amekanusha kuwahi kuwa na uhusiano naye.
 
Drama ya Agnes na hit maker wa ‘Duro’ imeibuka baada ya Tekno kufanyiwa mahojiano na mtangazaji wa Clouds Fm, Diva kupitia kipindi cha ‘Ala Za Roho’, ambapo alikanusha kabisa kuwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na video vixen huyo. Baada ya Tekno kukanusha, Masogange amesema kuwa Tekno anajua sababu zilizomfanya afiche ukweli kwa Diva, akimaanisha kuwa...
amedanganya. 
Masogange ameyasema hayo kupitia post ya Instagram ambayo baadae aliifuta, aliyokuwa akimjibu shabiki mmoja mwenye jina la Instagram @diva wolfgang aliyekuwa kama akimshushua kuwa Tekno amekanusha kuwa hajawahi kudate naye.
maso
Masogange aliandika; “Niko busy Na maisha yangu cna muda wa drama so plz hizo drama zenu hukohuko na why asiongee yote hayo b4 anajua kitu gani kilichomuuma that’s way anajishtukia ryt now niko next level “ . Pia mrembo huyo alipost picha za Tbt ambazo aliwahi kuzipost kipindi alipoenda Nigeria, moja akiwa kwenye studio ya Tekno.
tekno maso-2
na nyingine akiwa kwenye kitanda kinachofanana na kile kilichoko kwenye moja ya picha za Tekno mwenyewe alizoziweka Instagram.
tekno maso
tekno room-2
Tekno pia alipost picha ya chumba chake na kuandika, “#homealone”

Inawezekana Masogange hapa anajaribu kuthibitisha kuwa wamewahi kukutana faragha, ila yaliyofanyika kwenye kitanda hicho hayatuhusu…!

0 comments:

Post a Comment