Pages

Subscribe:

Sunday, April 3, 2016

BAGHDAD AMJIBU BABU TALE KWA BARUA HII NDEFU

Tale


Hivi karibuni rapper Baghdad alipishana na meneja wa Diamond, Babutale kwa kauli kwenye remix ya wimbo Mtazamo kuwa ana uwezo wa kuvifanya vyombo vya habari viwasahau wasanii. 


Kauli hiyo haikumpendeza Tale na kupitia mahojiano alimweleza kuwa kama rapper huyo anataka promo amfuate. Na sasa Baghdad ameandika barua ndefu aliyoitumia Bongo5 kuelezea mkasa huo. Well nimeona maelezo ya Babu Tale kuhusu kama ninahitaji promo niende akanipe. Jana ilikuwa siku yangu ngumu sana kwa kuwa wimbo wangu ulikuwa unatoka lakini wife naye hakuwa poa kiafya hali iliyopelekea kukataa mahojiano na vituo vingi vya radio nia yangu haikuwa...
kutokwenda wala si kana kwamba niliogpa kwenda kwa kumuhofia yoyote. Mziki wetu umetoka mbali na kila mtu analijua hilo, mimi binafsi nimechoshwa na kauli 3 


1. Mziki naudai hela nyingi saana
2. Haki utaipigania wewe wameshindwa kina sugu
3. Ishi nao wanavyotaka ili ufike.


Kweli muziki unaudai je utakulipaje au unataka kuuongezea madeni? Na ni kweli Sugu alianza kupigania haki ambayo mimi naendelea kuipigania ntakapoishia ataanza mwingine mpaka tufike, kwa kuwa hata Tanzania haikuletewa uhuru na baba wa taifa peke yake ni kazi ya watu wengi hivyo kufikia malengo ni kazi inayohitaji jitihada na juhudi za watu wenye lengo la kufika wanakotaka kwenda. 

Na hii ya 3 ya kuishi nao watakavyo ili ufike mwisho wa siku hutofika maana hutaenda kokote.

Babu tale anasema ya kuwa amenitoa kwenye group kisha akawatoa wasanii wake wote kasha naye kujitoa anapozungumza wasanii wake anamaanisha Diamond, Dogo Janja, Madee n.k na hawa ni kati ya wasanii wakubwa ambao amewanyima haki ya kuwa katika group linalotengenza umoja wa wasanii Tanzania ambapo leo hii wasanii tukisikia Dogo Janja kapata tatizo ni rahisi kwetu kumsaidia na kumfikia kwa uraisi tofauti na asipokuwa kwenye group.

Sasa nini suluhu ya hili suala, Tale anao uwezo wakutoa wasanii hata wote kwenye group alilolianzisha yeye nani atamuuliza? Hakuna lakini Tale hana nguvu ya kumfuta mwanachama yoyote katika chama chake cha sanaa. (TUMA) chama ambacho kilianzishwa kwa ajili ya kutetea kazi za wasanii wa mziki wa kizazi kipya.


Inasikitisha kuona hadi leo bado tuna wasanii wakubwa ambao hawako kwenye vyama vya miziki wanayofanya, mh waziri mkuu alizungumza na wachezaji wa mpira na kulisisitiza hili swala kwa sanaa yote kwa ujumla, mh raisi aisema hayuko tayari kufanya kazina msanii mmoja mmoja na hata mh waziri wa habari tamaduni na michezo amekuwa akitilia mkazo juu ya swala la wasanii kuwa ndani ya vyama. 


Mimi kama mimi nimejiunga Tuma na kugundua yapo mapungufu katika chama ambayo yalifanyika kibinaadamu sasa wakati wa kuitengeneza tuma tunayoitaka umefika, tazama sasa wasanii tunavutana kujua tunataka tulipwe au tusilipwe wakati cosota kwa miezi miwili imeshakusanya zaidi ya mil 500 na pesa hizo ni za wasanii lakini cha kushangaza kazi za wasanii zilizochezwa ni za changanyikeni wengine ni wanachama wa cosota na wengine si wanachama nani atalipwa hizo pesa kwa nini alipwe ni kwa kiasi gani yote hayo ni maswali ya kujiuliza lakini hatuwezi tukauliza wote kama kijiweni yanapaswa kuulizwa na chama.


Babu tale ninajua mchango wako katika mziki wasanii wengi wanakuogopa ni kweli ila kuwa msimamizi wa wasanii wanaofanya vyema ndani na nje haina maana ya kutoa ubinaadam wako na kusema hukosei maana hakuna mkamilifu, na yawezekana wakati mwingine unakosea pasipo kujua unakosea, mfano kauli ya kusema umetoa wasanii wako wote kwenye group kwangu imenipigilia mstari kuwa hata tukiwasikia leo hii wasanii wako wanaongea jambo au wamesimamia upande flani wa shilingi wewe unahusika kwa asilimia kubwa, sasa mimi ushauri wangu mkubwa kwako na kwa yeyote ambae anafanya kazi ya sanaa bila kujali nafasi na nguvu aliyonayo ni kwamba kama hajajisajili (TUMA) ajisajili mara moja ili tutengeneze mwamvuli utakaotukinga na maharamia wanaoiba kazi zetu miaka mingi. 


Mimi sina ukorofi na wewe na sikuwa na lengo baya na wewe na si dhihaka kukueleza ya kuwa una nguvu ya kuanya media hous wanidharau hiyo ni hali halisi na nakuomba unapoambiwa jambo ukalipima ukagundua lina ukweli jaribu kulifanyia kazi na usilikimbie, mwisho nikushukuru kwa kuendelea kufanya kazi na wasanii na nikuahidi lolote nitakaloona linafaa kukwambia kama sifa nitakupa utakapopatia bila kificho na utakapokosea nitakuambia na ninaimani hutaona ninatafuta promo maana nyimbo yenyewe ya mtazamo iisha heat tangu zamani.


Kwa msanii ambae anaimba mziki wa kizazi kipya sehemu salama ni (TUMA) na niwashauri wasanii ambao bado siku si nyingi mambo yatabadilika wan je wan je na wa ndani wandani haitaleta maana kuona Baraka da Prince hatambuliki ki sanaa kisa si mwanachama wa chama chochote. Kwa anaetaka kujiunga na chama cha tuma anaweza kunitafuta kwa number 0652 89 48 71 nitamuelekeza akhsanteni

0 comments:

Post a Comment