Wasafi
Classic Baby ama (WCB) kama inavyofahamika na wadau wengi wa burudani ni record
label ambayo iliasisiwa na gwiji wa muziki nchini Tanzania Nasibu Abdul(Diamond
Platnumz)kama anavyopenda aitwe na mashabiki wake ikisimamiwa kwa karibu na
wanaoaminika kuwa ni wasimamizi bora kabisa wa kazi za muziki wa kizazi kipya
kwa sasa nchini Tanzania ambao ni Babu Tale, Mkubwa Fella pamoja na Sallam SK.
Kwa
kiasi kikubwa label hii imefanikiwa kupush sanaa ya Tanzania na kuipeleka mbele
zaidi sio tu kwa upande wa waimbaji bali hata...
dancers,wapiga picha pamoja na
producers.
Ukimuondoa
Diamond Platnumz ambaye ni boss, currently record label hii ina wanamuziki
wawili ambao ni Harmonize kijana kutoka kijiji cha Chitoholi wilayani
Tandahimba mkoani Mtwara anayefanya poa na hit song yake aliyomshirikisha bosi
wake (Bado)pamoja na kijana mwingine aitwaje Raymond(Rayvanny) ambaye kiasili
ni mwenyeji wa mkoa wa Mbeya anayesumbua pia mtaani na ngoma yake (Kwetu)
iliyomtambulisha rasmi katika industry hii.
Lakini
kwa siku za hivi karibuni kupitia media mbalimbali kumekuwepo na tetesi ambazo
zinamhusisha msanii A list katika kiwanda cha Bongo Flava, Rich Mavoko kuwa
signed katika label hii.
Rumors ambazo ziliasisiwa na boss wa label hii Diamond Platnumz alipofanya mahojiano na (AYOTV) na kueleza kuwa Mavoko alitakiwa awe signed na Wasafi kabla hajatoa hii ngoma yake mpya(Naimani)
“Ilitakiwa
itoke under management ya Wasafi lakini kuna vitu vilichelewesha deal hiyo,”
alisema Diamond.
Tetesi
hii baadaye ilikuja kuongezwa nguvu na Harmonize mmoja wa wasanii walio chini
Wasafi pale alipothibitisha kuwa Wasafi ina wasanii watatu ambao wako signed
akiwemo yeye mwenyewe,Raymond pamoja na Rich Mavoko, tetesi ambayo baadaye
ilikuja kukanushwa na Sallam, meneja wa Diamond pamoja na Rich Mavoko mwenyewe
Licha
ya kuwepo na ukweli juu ya mazungumzo yaliyofanywa kati ya management ya wasafi
pamoja na Rich Mavoko, bado mimi sitaki kuamini kukubali kuwa Mavoko anaweza
kweli comfortably kuwa under Wasafi management inayoongozwa na Diamond ingawa
hakuna shaka kuwa deal hii inaweza kuwa ni yenye tija kwa wote wawili kutokana
na resources ambazo wawili hawa wanazo.
Tukumbuke
kuwa Diamond ana connection kubwa ya nje pamoja na fund ya kuinvest kwa Mavoko
huku Mavoko yeye akiwa na talent kubwa ya uimbaji pamoja na utunzi usio na
shaka lakini bado ninapata mashaka makubwa na imani yangu inanifanya
nijiridhishe kuwa hii deal haiwezi kukamilika kutoka na makandokando haya:
1.
NAFASI YA RICH MAVOKO KATIKA MUZIKI WA BONGO FLAVA
Hapana
shaka kuwa Rich Mavoko ni miongoni mwa A list katika wasanii wa Bongo Flava na
anayo fan base yake ambayo pia ni kubwa ingawa hana mafanikio ya kutisha sana
katika industry hii.
Kuna
time ambayo Rich alikuwa nyuma ya Diamond akiwa kama mshindani wake mkuu
kutokana na style ya muziki wao hali iliyokua inapelekea kutokea kwa
misunderstanding za mara kwa mara kati yao hadi kutuhumiana uchawi. Sasa basi
Mavoko kwenda kusign katika label iliyo chini ya aliyepata kuwa hasimu wake
ambaye anaamini ana kipaji kikubwa pia ni kama ”Kujishusha”na
“Kujidhalilisha”ingawa kwa sasa ukweli ni kwamba hawa watu hawako tena katika level
zinazofanana.
2.UWEPO
WA BABU TALE NA MKUBWA FELLA
Hakuna
ubishi kuwa kwa kiasi kikubwa muziki wa Bongo Flava umeshikiliwa mikononi mwa
hawa jamaa wawili. Wanaaminika kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuwa na uwezo wa
kusema huyu “AWE huyu ASIWE” na mara nyingi wamekua wakigubikwa na shutuma
mbalimbali kutoka kwa wasanii kama “Unyonyaji” na shutuma nyingine nyingi
ingawa pia tunafahamu hakuna binadamu mkamilifu.
Watu
hawa wanapenda kuheshimiwa kwa kiasi kikubwa na mara nyingi hupima nidhamu ya
msanii kwa kumpa msoto sanaa rejea kwa Raymond na wengine msoto ambao unahitaji
uvumilivu na busara ya hali ya juu kuweza kuuvuka kitu ambacho kwa hulka na
tabia ya Mavoko hawezi kukivumilia na kuna uwezekano mkubwa wa kupishana
Kiswahili na hawa watu wawili na kwa kulitambua hili ninaamini hii ni miongoni
mwa sababu zinazofanya deal ya Mavoko na Wasafi kuwa ngumu zaidi.
3.KUKOSA
UHURU WA KUFANYA MAMBO BINAFSI KWA WAKATI
Labda
niseme tu kuwa Rich hajaishi na kukulia katika maisha au mazingira
yanayomuhitaji kufuata utaratibu zaidi kama ambavyo wasanii walio chini ya
label ya Wasafi wanavyoishi.Inasemekana ukiwa Wasafi ni kazi nonstop haina ile
kuhang kwenye viwanja vya starehe kama vile clubs na maeneo yanafanana na hayo
mara kwa mara na muda mwingi wanautumia wakiwa ndani(studio) wakirekodi ngoma
au kufanya mazoezi. Kifupi maisha ya wasafi ni kama academy.
Kwa
wasanii wachanga na wanaotafuta tobo kama Harmonize na Raymond hii inaweza
isiwe kazi ngumu kwao hata kidogo lakini kwa msanii mkubwa wa aina ya Mavoko
lazima kutakua na ugumu fulani kwakuwa anaweza kukosa ule uhuru wake wa
mwanzoni wa kuhang na washkaji au kupata time ya kufurahi na baby wake na vitu
kama hivyo
4.
DIAMOND PLATNUMZ MWENYEWE
Siamini
kama kuna kitu kigumu kama kumsimamia mtu mliye katika industry moja mfano
muimbaji kumsimamia muimbaji mwenzake na hasa ikiwa huyo muimbaji
(msimamiaji)bado anafanya muziki wa ushindani.
Hapa kuna mambo yanaweza kutokea msimamiwaji kushindwa kupiga hatua,msimamiaji kushuka thamani yake(kimuziki)au wote kushindwa kuendelea.
Imagine Diamond na Mavoko wote wanawania tuzo lets say wimbo bora wa mwaka au msanii bora wa kiume na Mavoko akabeba hiyo tuzo ushajiuliza au kufikiria ni nini kinaweza kutokea?
Inaweza
isiwe shida kubwa kwa wenzetu ambao wametutangulia na kuwa na exposure kubwa
lakini haiwezi kuwa rahisi kwetu sisi ambao hatuna ukomavu na kisanaa(boss
kwanza wengine wanafuata).Rejea ugomvi wa Bob Junior na Diamond Platnumz.
5.DONGO LA RICH MAVOKO KWA HARMONIZE
Wakati
Harmonize alipoupa nguvu uvumi wa Rich Mavoko kusign Wasafi, Mavoko alionekana
kama kumjibu Harmonize kwa njia ambayo sio rahisi kuigundua pale alipotumia
page yake ya Instagram kupost maneno haya, “Ukipata nafasi ya kuongea ongea vya
maana ukiongea visivyo na maana utaonekana hauna maana,”ambayo yanaashiria kuwa
ni dongo la moja kwa moja kwenda kwa Harmonize ambaye ni wazi anaonekana kuwa
msanii kipenzi wa Diamond.
Ni
wazi kuwa vijembe kejeli na majivuno ya Mavoko ni vitu ambavyo vinanifanya
niamini kuwa deal yake na Wasafi haiwezi kutokea. You can prove me wrong
baadaye kama ikitokea lakini kwa sasa msimamo wa kichwa changu ni huu.
0 comments:
Post a Comment