Msanii mkongwe wa muziki, Mr Blue amesema amepata management mpya kutoka Afrika Kusini itayokuwa inasimamia muziki wake.
Akizungumza
katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Mr Blue amesema management hiyo tayari
imeshamtafutia kobalo na msanii mkubwa wa Afrika. “Kwakweli
mwaka huu nashukuru umeanza vizuri kwangu kwa sababu kwanza nimepata
‘management’ nzuri sana ambayo ipo ‘South Africa’ jamaa ni Watanzania lakini...
wanaishi huko wameuona muziki wangu wakaniambia muziki wangu mzuri ila nimekosa
‘kampani’ ya watu wa kunisapoti kwahiyo wamejitolea kunisaidia na mwaka huu
nitafanya video kubwa na msanii mkubwa wa Afrika,” alisema Blue.
“Kwa
hiyo Mungu akisaidia mwaka huu nitafanya video kubwa na msanii mkubwa wa Africa
sitaki kumtaja mapema. Kwa hiyo wimbo utaandaliwa Afrika Kusini pamoja na video
japo kuwa kuna nyimbo kadhaa nimeshazirekodi nitazitoa kwanza alafu hiyo ya
kimataifa itatoa katikati ya mwaka huu au mwishoni,” aliongeza Blue.
0 comments:
Post a Comment