Pages

Subscribe:

Sunday, April 3, 2016

QUICK ROCKA KUACHIA WIMBO NA VIDEO BAADA YA WIKI MBILI

e3c810802893_800431659995647_1858303498_n


Quick Rocka ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo Fleva ambao nyimbo zao ziliwahi kuvujishwa.

Quick Rocka ni kati ya wasanii wachache wa Bongo wanaomiliki studio ‘Switch Recs’ lakini pia ni msanii aliyepata bahati ya kuwa msanii wa mwisho ya kufanya collabo na marehemu Ngwair, kwenye wimbo ‘My Baby’.

Akiongea na Bongo5, Quick Rocka amesema, “Niliamua kutoachia video ya ‘Nakupenda’ kwa sababu kuna mtu aliivujisha wimbo huo kabla haujatoka na haukuwa kwenye plan zangu. Wiki mbili zijazo nitaachia wimbo wangu mpya ukiambatana na video yake, lakini...
pia kuna wasanii kadhaa nimewashirikisha kwenye wimbo huo.” 

Wimbo aliopanga kuuachia, umetayarishwa kwenye studio zake ya Switch Records chini ya producer Lufaa.

0 comments:

Post a Comment