Friday, August 18, 2017
AMBER LULU: FAMILIA YANGU HAIFUATILII MASWALA YA MTANDAO
Msanii wa muziki na video vixen Bongo, Amber Lulu amedai kuwa familia yake haifuatilii mitandao hivyo yupo free kujiachia kwa kuweka picha anazotaka.
Video Vixen huyo ambaye ameingia kwenye muziki wa Bongo Flava na kutoa ngoma ‘Watokoma’ ambayo alimshirikisha Country Boy, ameiambia Leo Tena ya Clouds Fm kuwa hata familia ikiona picha zake...
hamna tatizo.
“Familia yangu hawafatilii mitandao ya kijamii na hata wakiona picha zangu kwa sasa wanaelewa nini nafanya. Siyo kila kitu tunachoposti kwenye mitandao ya kijamii ndivyo maisha yetu tunayoishi” amesema Amber Lulu.
Kabla ya kuingia katika muziki na kutangaza kuachana na u-video vixen, Amber Lulu alishatokea kwenye video kama Inde ya Harmonize na Dully Sykes, Usimsahau Mchizi ya Roma na Moni n.k.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment