Pages

Subscribe:

Friday, August 18, 2017

ALIKIBA KUMLIPA DIAMOND KWA KUACHIA NYIMBO TATU KWA MPIGO

Msanii Alikiba ambaye yupo kimya kwa muda mrefu ameamua kukata kiu ya mashabiki wake na kumaliza hasira zao kwa kushusha ngoma tatu mfululizo pindi atakaporejea Tanzania kutokea nchini Marekani alipokwenda kwa ajili ya kufanya show. 

Siku mbili zilizopita Alikiba kupitia mitandao yake ya kijamii alianza kuweka post ambayo ilionyesha ni ishara ya ujio wake mpya baada ya kuweka 'post' iliyokuwa na jina la 'Kipusa' na kuaindikia...
maneno kuwa "Wananiita Kipusa' baada ya siku moja aliweka nyingine iliyokuwa inasema 'they call me a heartbreaker" hali ambayo ilianza kuwachanganya mashabiki wake wengine wakidhani kuwa ni mistari kutoka kwenye wimbo huo. 

Lakini siku moja mbele aliweka post nyingine inayosema 'Pasua Kichwa' hali ambayo ilizidi kuongeza maswali mengi kwa mashabiki wake, lakini mdogo wake na Alikiba anayefahamika kwa jina la Zabibu ameweka wazi kaka yake Alikiba ataachia kazi tatu kwa mpigo na kuwataka mashabiki wakae mkao wa kula pindi atakaporudi kutoka nchini Marekani ataachia kazi hizo. 

Alikiba siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Agosti atakuwa akikiwasha nchini Marekani katika mji wa New York ambapo atakuwa na wasanii wengine kibao kutoka Afrika wakiwepo P Square, 2 Baba, Tiwa Savage pamoja na  Cassper Nyovest

0 comments:

Post a Comment