Rapa Rashid Makwiro 'Chid Benz’ amekamatwa akiwa na wenzake saba kwa
tuhuma za kukutwa wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya aina ya
Heroine mapema wiki.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amethibitisha kukamatwa kwa
watuhumiwa hao ambapo amesema kuwa walikamatwa Agosti 12 mwaka huu saa
11.50 jioni wakijihusisha na...
uuzaji wa dawa za kulevya.
Amesema jeshi la polisi limefanya msako
wake na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa katika eneo ambalo
linajihusisha na uuzaji wa dawa hizo.
“Chid Benz na wenzake wapo
kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi na pindi
utakapokamilika tutawafikisha Mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa
zimepelekwa kwa Mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za
kulevya zilizokamatwa”, alisema Hamduni.
Hamduni amesema jeshi hilo linafanya
msako liweze kubaini mtandao mzima unaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya na watumiaji ili kuhakikisha wote wanachukuliwa hatua na
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Pamoja na hayo tukio hilo la kukamatwa
kwa Chid Benz limetokea ikiwa ni muda mfupi tangu arudi kwenye muziki na
kukuri kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zilimfanya
akapotea kwenye 'game'.
Hata hivyo kumbukumbu zinaonyesha kuwa
hii siyo mara ya kwanza kwa msanii huyo kukamatwa akijihusisha na dawa
za kulevya, itakumbukwa Oktoba 2014, Rapa huyo alikamatwa uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jiji la Dar es
Salaam akiwa na dawa za kulevya, akijaribu kuvuka nazo kwenda mkoani
Mbeya kushiriki tamasha la 'Instagram Party' akiwa na msanii Shetta.
0 comments:
Post a Comment