Msanii na mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva ambaye pia ni mmoja wa
wasanii wanaounda kundi la SSK, Cjamoker amesema ilibakia kidogo ajitoe
uhai wake kipindi alipokuwa amelazwa katika chumba maalum cha wagonjwa
mahututi ICU.
Cjamoker
amebainisha hayo leo wakati alipokuwa anazungumza baada ya kuulizwa swali na mmoja
wa waongozaji kuhusiana na maisha yake aliyoyapitia
katika...
kuumwa.
"Nilitaka kujiua nilipokuwa
ICU, maana kuna siku nilikuwa naota ndoto kama hospitali imevamiwa na
madudu halafu yakawa yanauwa 'Nurse' sasa mimi kwa kutaka kujiokoa
nikajikuta najitoa mipira niliyokuwa nimewekewa kunisaidia kupumua na
kusababisha hali ya taharuki kwa madaktari pindi walipokuja, kwani
madaktari hao baadhi yao walikuwa hawawezi namna ya kuirudisha mipira
hiyo hivyo ilibidi waniwekee dripu la kawaida mpaka asubuhi ndipo
nilipokuja kuwekewa mipira hiyo na madaktari wengine", amesema Cjamoker.
Pamoja na hayo, Cjamoker ameweka wazi
jambo ambalo lilimpelekea kuumwa kwa kipindi kirefu na kushindwa kufanya
kazi ya aina yoyote ile na mwisho kuwa mtu wa kulala tu.
“Kitu kilichokuja
kunisababishia mimi kuumwa ni kutokula kwa wakati, nilikuwa napitiliza
kutokula kwa wakati, unajua kazi zangu ni production nakuwa busy,
wakaniambia utumbo umetoboka, umejikunja na pia waligundua na henia, pia
wakaniambia matumizi ya pombe ingawa nilikuwa situmii sana”, alisema Cjamoker.
Kwa upande mwingine, Cjamoker amesema
anawashukuru wazazi wake kwa upendo waliyokuwa wamemuonyesha wakati
alipokuwa yupo kitandani kwa maana kuna vitu vingine alikuwa hawezi
kuvifanya yeye kama yeye.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment