Meneja Mkubwa Fella ambaye pia ni mingoni mwa wale wanaomsimamia
Diamond Platnumz amesema hilo haliwezi kumzuia kufanya kazi na Alikiba, Kutokana na ukaribu wake na Diamond mashabiki wengi wamekuwa
wakidhani kuwa yeye ni team Diamond, hata hivyo ameeleza katika kazi
hakuna utimu.
“Kwanza ukae ukijua sijawahi kusema
sifanyi kazi na mtu yeyote, Alikiba mimi ni mwanangu wa dhahabu, ni
mwanangu wa gold wala usiseme kuna hiki na hiki japokuwa...
wanasema
chawa, basi chawa waje vizuri kwa sababu mimi ndiye meneja wa kwanza
katika muziki huu sina pingamizi kusema nitafanya kazi na mtu niogope
kufanya kazi na mtu,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.
“Wote ni wanangu mimi ni mkubwa na wanae, kwa hiyo Alikiba ni
mwanangu, haijawahi kuonekana hata siku moja mimi na Alikba
tunagombana,” amesema Fella.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment