Pages

Subscribe:

Thursday, August 10, 2017

MWIGIZAJI ALIYE JITANGAZA KUZAA NA HAMISA MOBETO ASHAMBULIWA


Mshindi wa milioni 50 za Tanzania Movie Talent, Dennis Louis amesema mtoto wa Hamisa ni wake sio wa Diamond kama watu wanavyodai kauli ambayo imewafanya madau wengi katika mitandao ya kijamii kupingana na kauli hiyo huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kudai kwamba ametumwa.

Muigizaji huyo amekuwa akipost vitu mbalimbali kupitia mtandao wake wa Instagram kujaribu kuthitisha...
kwamba mtoto huyo ni wake.

“Mengi yamesemwa nimevumilia vya kutosha mwenye mzigo nadhani mshanijua!! Kabla hamjaandika mambo zenu muwe na evidence za kutosha!!. Basi wenye wivu watasema Photoshop shubaaamit!!! #babajunior #comingsoon” amepost picha akiwa na Hamisa,” aliandika muigizaji huyo Instagram.

Katika post nyingine yenye picha yake na Hamisa Mobetto ameandika, “Siku tuliyomtengeneza junior wetu mimi na mama Dee pale magomeni usalama. Hotel siitaji..kila mtu apambane na huba lake…kuna mwenye tatizo huko!? Kama yupo kufwaaaz you know!!,”

Hata hivyo imebainika kuwa picha zote alizoweka Dennis akiwa na Hamisa sio halisi bali zinadaiwa kutengenezwa. Mobetto hajaweka wazi mtoto wake huyo ni wa nani huku wadai wa mambo wakidai mtoto huyo ni wa Diamond.

0 comments:

Post a Comment