Msanii wa bongo fleva, Nuh Mziwanda amefunguka na kudai hataki kusikia
tena habari za wanawake kwa sasa kwa kuwa yeye ni 'single boy'. Mziwanda
ameeleza hayo kupitia kipindi cha 5seleKt kutoka EATV baada ya kupita
siku chache tokea aachane na mke wake waliofunga ndoa anayefahamika kwa
jina la Nawal.
"Sasa hivi nipo 'single boy' sitaki mambo ya wanawake yaani staki hata kusikia",amesema Mziwanda. Hata hivyo, Nuh amesema japokuwa wameachana na mke wake lakini bado...
anaendelea kumtunza mtoto wake kwa kila hali.
"Nilitamani sana mtoto wangu
ning'ekaa naye mimi 'since' yupo mdogo lakini nashindwa kufanya hivyo
kwa sababu ya umri wake haujifikia kukaa na baba kwa hiyo nimemuachia
mama yake kwa sasa lakini kama nikiona mwanangu wanamfanyia vitu ambavyo
si sawa kwangu nitaenda kumchukua nikae naye mimi mwenyewe", amesisitiza Mziwanda.

Mtoto wa Nuh Mziwanda aliyepewa jina la Anyamile
Kwa upande mwingine, Nuh amedai amempa
muda wa kumchunguza mzazi mwenzake kama ataweza kuishi na mtoto wao
vizuri na endapo atabaini kasoro zozote basi atamchukua na kukaa naye
mwenyewe.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment