Rapa Roma Mkatoliki amewaacha njia panda mashabiki wake kwa kile
alichokiimba katika wimbo wake mpya wa 'Zimbabwe' ambapo watu wengi
wameshindwa kutafsiri mashairi yalitumiwa humo huku wengine wakiangua
vilio baada ya kuona video hiyo.
Katika
wimbo huo Roma Mkatoliki amejaribu kuhusisha matukio mbalimbali ya
kisiasa pamoja na lile la kwake kubwa la kutekwa ambapo hii ndiyo kazi
yake ya kwanza tokea ule mkasa wake wa kutekwa kuisha na kusababisha...
maumivu mengine makali kutoka kwa mashabiki zake baada ya kuona 'video'
yake mpya iliyojaa hisia kali za maumivu.
Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa
'youtube' alioweka video hiyo mpya watu zaidi ya 668 wametoa maoni yao
jinsi walivyoupokea ujio mpya wa Roma na hizi ni baadhi tu ya zile
zilizoandikwa na mashabiki wa Roma.
Pharergy Ramson: "Roma
ukienda Zimbabwe harakat atazifanya nani 'but' ngoma iko poa hujawahi
kuniangusha ila umebadirika kidogo mzee. Nadhan kwenye hii ngoma umejibu
maswali ya watu wengi sana kipindi unafanya 'show' pale 'Dar live'
nilitamani urudie hii nyimbo 'but' sikuwa na uwezo ila umefanya vizur."
Blandina Bilau: "Simjui sana
Roma wala kufuatilia nyimbo zake lakini huu wimbo umeniliza, 'message'
imefika jipe moyo. Mtetezi wako Mungu aendelee kukutetea"
Arthur Oyaro: "Duuh 'so sad' na utu uzima huu machozi nimeshindwa kuyazuia,'thank' pia kwa kunifikirisha. Viva Roma viva''
Mdachi Classic: "Nimefatilia
'comment' nyingi sana ila sijaona hato komenti inayozungumzia vibaya
hii ngoma zaidi ni za upendo na za kuumizwa tu. 'In short' hii imetugusa
sana pole sana kaka yupo mungu hakimu wa yote".
Ibrahim Utenga: ''This song reflects the real prevailing situation, it's very sensitive song, congratulations to you brother, God save you "
Ndongo Nyambalya: "Nina
wasiwasi wewe Mkatoliki hicho siyo kichwa ni semi-computer, kwenye
Mungu wa John na Daud hapo nimefikiria hadi najikuta nurudiarudia
kusikiza, U deserve bro! Gat u! 100".
Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki
amemwagiwa sifa kedekede na mashabiki zake ambao walikuwa wamemisi
kusikia na kuona kazi zake kwa kipindi kirefu tokea alipopatwa na mkasa
wa kutekwa miezi michache iliyopita na kuweza kurudi katika uhalisia
wake bila ya kuhofia jambo lolote litakaloweza mtokea tena mbele yake
kwa ukali wa tungo zilizojaa za kufikirika.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment