BOB
na Micharazo wameanza ziara ya nchi nzima waliyoipa jina ‘Biz Kwenye Game.’
Ziara hiyo inaanza Ijumaa hii mjini Mtwara.
Akiongea
na Bongo5, Nyandu Toz amedai kuwa tangu BOB na Micharazo waungane pamoja
hawajahi kufanya ziara ya pamoja na hivyo mwaka huu wameamua kuwapa mashabiki
kile walichokisubiri kwa muda mrefu. “Mwaka
huu 2016 tumeamua kuacha...
shughuli zote, Kabayser aache mambo yake, Becka aache
shughuli zake, mimi niache shughuli zangu tuwe busy kwenye game.
So ndio maana
hii tour imeitwa Bob & Micharazo: Busy kwenye Game,” amesema Nyandu. Amesema
wameamua kuanza mikoa ya Kaskazini ambapo Ijumaa hii watakuwa Mtwara, Jumamosi
Masasi na Jumapili Lindi.
Kwa
upande mwingine Nyandu amesema BOB na Micharazo ni kundi ambalo limedumu kwa
muda mrefu bila migogoro na kwamba mwaka huu wameamua kuwapa vitu vingi zaidi
mashabiki wao.
0 comments:
Post a Comment