
Vyombo vya habari nchini Zimbabwe vimeripoti kuwa mke wa Rais wa
Zimbabwe, Robert Mugabe, Bi Grace Mugabe amerejea nchini humo kutoka
Afrika Kusini licha ya kutafutwa na jeshi la polisi kujibu mashtaka ya
kumshambulia Mwanamitindo Gabriella Engels katika hoteli moja jijini
Johannesburg.
mahakama nchini humo.
Mwamitindo Gabriella Engels 20, alimshutumu Bi Mugabe kwa kumpiga baada ya kumkuta akiwa na watoto wake wawili wakiume lwenye chumba kimoja cha hoteli nchini Afrika Kusini mtaa mmoja wa kifahari wa Sandton, kaskazini mwa mji wa Johannesburg.
Mawakili wa Gabriella Engels mwanamke ambaye anamshtaki Bi Mugabe kwa kumjeruhi, wanasema kuwa mteja wao alipewa pesa kuachana na kesi hiyo lakini akakataa.
Bi Engels, alionekana kwenye mkutano wa waandishi waahabari siku ya Alhamisi akiwa na bendeji kubwa kwenye uso wake huku Bi Grace Mugabe akikataa kufika mahakamani baada ya kushtakiwa wiki jana, akidai kuwa na kinga ya kidiplomasia.
Hata hivyo Mamalaka za Afrika kusini zimekanusha madai hayo kwamba Bi Grace Mugabe ana kinga ya kidiplomasia.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment