Mwanamama aliyewahi kuwika miaka ya nyuma kunako tasnia ya filamu Bongo, Lucy Komba, amejikuta akipoteza sifa ya mwanamke mvumilivu baada ya kutoa povu kwenye ukurasa wake wa Instagram, chanzo kikiwa ni Hamisa Mobeto.
Nyongo ya mwanamama huyo ilitibuka baada ya kuona baadhi ya watu katika
mitandao ya kijamii wakimshambulia kwa maneno Hamisa Mobetto, kuhusiana
na mtoto aliyejifungua hivi karibuni, hali iliyompelekea...
kukumbuka
vichambo alivyowahi kuvipokea kuhusiana na ndoa yake.
“Samahani lakini kimenichoma, Mabogas ya TZ yanamponda Mtanzania mwenzao, yanamsifia Bogas,
sijui yanadhani yatapewa ule urithi, mbona Waganda hawambabaikii?
Acheni umaskini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja
karanga mojamoja ya bure?”
Na baada ya posti hiyo akaona haitoshi muda mfupi baadaye akaposti tena
picha ya Hamisa akiwa na mtoto wake wa kwanza, Fantasy, na kuandika
maneno yafuatayo:
“Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda
wakati roho zinawauma, unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku
unatabasamu, wale wanaoniponda ningekuwa mzalendo nisingeolewa na Mzungu;
“Ndiyo nimeolewa na Mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na
tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wa Kiafrika, kwa hiyo
lazima mjue kutofautisha A na B;
“Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataarifu
halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia Insta na
kuzizungusha bado hajawapa taarifa za kunichamba;
“Ukweli unauma mmepewa ukweli kwa huyo mgeni wenu aliyenenepesha
miguu, kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia, chambeni tu mniongezee
Followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa Bongo
unatokana na vichambo” ameandika Lucy Komba.
Thursday, August 10, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment