Pages

Subscribe:

Thursday, August 10, 2017

MONI: MASHABIKI WASIDHANIE KUWA NTAIMBA TUKIO LA KUTEKWA

Msanii wa Hip hop anayewakilisha Kanda ya Kati, Moni Cetrozone amewataka mashabiki zake kutomfikiria yeye kuja kuimba siasa kutokana na matatizo ya utekwaji aliyoyapata Aprili 05, 2017 akiwa na Msanii Roma Mkatoliki. 

Moni amefunguka na kusema atashangaa sana kuona kama kuna shabiki anayesubiri yeye aimbe nyimbo za kuhusu...
tukio la kutekwa kwani ni kitendo ambacho hajawahi kukifanya tangu anaanza kufanya muziki. 

"Mimi nyimbo zangu nyingi zinahusisha maisha niliyoshi huko Majengo Sokoni, changamoto za maisha ya watu wangu wanazopitia pamoja na yale niliyoishi.  Hata ukisikiliza wimbo nilioshirikiana na Roma nimeimba maisha na siyo siasa. Mashabiki wasidhanie kwamba nitaimba matukio yale lakini nachotaka tu kuwaambia wakikusanya nyimbo zangu zote wanaweza kutengeneza albamu" Moni

Kuhusiana na kumshirikisha baraka katika wimbo wake mpya Moni amesema ni suala la kibiashara ndilo alilozingatia haswa kwa msanii kama Baraka The Prince ambaye tayari ana mashabiki wa kutosha.

"Naamini sana kolabo kwani hata kolabo ya Roma 'Usimsahau mchizi ni wimbo ulioniweka kwenye nafasi nzuri hivyo hata hii ya Baraka najua utanifikisha sehemu nzuri zaidi" - alisisitiza Moni

0 comments:

Post a Comment