Kutokana na kuwepo kwa madai ya Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kuchangia
kuvunjika kwa ndoa ya mpenzi wake wa zamani, Naftal Mlawa ‘Nuh
Mziwanda’, msanii huyo wa muziki na filamu ameibuka na kusema mambo hayo
hayamhusu.
Vyanzo mbalimbali kwa nyakati tofauti vimedai kuwepo kwa uhusiano wa
kimapenzi baina ya wapenzi hao wa zamani licha ya Nuh kuwa katika ndoa,
kitu kilichokuza mgogoro wa... wanandoa hao ambao wamejaaliwa kupata mtoto
mmoja wa kike, kiasi cha mwanamke kuamua kutimka.
Baada ya kupata habari hizo, Za Motomoto News ilimtafuta Shilole ambaye
alijibu kwa kifupi; “Kila mtu apambane na uhusiano wake, pia mambo ya
ndoa kuvunjika hayanihusu.”
Naye Nuh akasema; “Migogoro ndani ya ndoa ni kitu cha kawaida, kuhusu
Shilole siyo kweli, Nawal alikuwa na mambo yake hivyo alikuwa anatafuta
kisingizio cha kuondoka, sijampa talaka bali aliamua kuondoka mwenyewe
hivyo ninachoweza kusema ni kwamba namshukuru Mungu ninaendelea kupumua
hayo mengine ni ya ziada tu, kikubwa uhai.”
Wednesday, August 9, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment