Pages

Subscribe:

Wednesday, January 31, 2018

LIONEL MESSI KUICHEZEA TIMU YA DAVID BACKAM LIGI KUU LMS

Mess Ampa Ahadi David Beckham
Baada ya nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Beckham kutangaza kuwa yupo mbioni kuanzisha klabu ya soka, nyota wa Barcelona Lionel Messi amempongeza.

Messi ametoa pongezi hizo kupitia video fupi ambapo pia amemwambia Beckham kuwa huenda miaka michche ijayo akaungana naye kuchezea klabu hiyo.

''Kwanza nikupongeze sana kwa hatua hiyo mpya unayoianzisha, naamini kila kitu kitakwenda sawa, na...

huwezi jua miaka michache ijayo naweza kupokea simu kwaajili ya kuchezea klabu hiyo'', ameeleza Messi katika video hiyo.

Hivi karibuni nyota huyo aliyekipiga na vilabu kadhaa ikiwemo AC Milan na PSG ameweka wazi kuwa tayari wazo lake la kuanzisha timu itakayoshiriki ligi kuu ya Marekani (MLS) ameshaanza kulifanyia kazi na makao makuu ya timu hiyo yatakuwa jijini Miami.


David Beckham ambaye ni raia wa Uingereza alicheza kwa mafanikio katika soka ngazi ya klabu kabla ya mwaka 2007 kutimkia nchini Marekani kwenye klabu ya LA Galaxy.

0 comments:

Post a Comment