Pages

Subscribe:

Friday, January 26, 2018

RAIS JPM AMFUTA MACHOZI WASTARA KWA KUMCHANGIA MIL 15


Leo January 26, 2018 katika mitandao ya kijamii zimesambaa picha zinazomwonyesha Mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu Ngusa Samike akiwa amemtembelea muigizaji wa Bongo Movies Wastara Juma nyumbani kwake anayeumwa na kumpatia kiasi cha Tsh milioni 15.

Inaelezwa kuwa pesa hiyo imetolewa na Rais John Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli ili zimsaidie katika matibabu. Samike pia amemkabidhi Wastara mchango wa...
Tsh milioni moja na laki tisa kutoka kwa wasaidizi wa Rais.

Wiki iliyopita Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe pamoja na wawakilishi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walimtembelea Wastara na kumkabidhi mchango wa Tshs milioni moja.

Siku za hivi karibuni Wastara amehojiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kusema kuwa wasanii wenzake wa filamu hawamjali hata kumchangia fedha kwa ajili ya matibabu yake.

0 comments:

Post a Comment